Katika kuelekea uchaguzi wa marudio zanzibar Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi visiwani humo Juma salum Jecha ametoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusiana na maandalizi ya uchaguzi na tume ilivyojipanga,
Akizungumzia maandalizi hayo amesema yanaenda vizuri ikiwa ni
pamoja na uteuzi wa wasimamizi wa uchaguzi, upangaji wa vifaa,
mawasilaino na vyama na uchapishaji wa dafatri na mafunzo na wagombea
kuanza kupatiwa ulinzi na haki zote kwa mujibu washeria huku akielzea
karatasi za kura amabzo zinachapwa nje zinatarajiwa kuwasili mapema
mwezi ujao.
Kwa mujibu wa tume ya uchaguzi vyama amabvyo vimethibitisha
kushiriki ni pamoja na CCM, TADEA, ADC, CCK, AFP, SAU, TLP, huku CUF,
NRA, CHAUMA, DP, Jahazi asilia na ACT Wazalendo ambao mgombea wake
Khamis Lilla ametangaza kugombea huku chama chake kikimufukuza
uanachama.
Msimaamo huo wa tume umetolewa na mwenyekiti wa tume hiyo ya uchaguzi ya
Zanzibar Jecha Salum Jecha katika taarifa yake kwa vyombo vya habari
ambapo amesema kuna utaratibu wakujitoa na kwa mujibu wa sheria na
kanuni za uchaguzi hakuna chama kilichofuata kanuni ikiwa ni pamoja na
wadhamini wawagombea kutangaza kuondoa udhamini wao, hivyo wagombea wote
wa urais, uwakilshi na udiwani wote bado ni halali.
JE UNA MAONI GANI KWA MSIMAMO HUU WA ZEC?USIACHE KUCOMENT THEN SHEA NA WANA.