Rubani wa ndege ya makamu wa raisi Nchini kenya alinaswa na kamera akimtusi askari polisi aliyekuwa kwenye eneo lake la kazi,Taarifa zinaeleza kuwa rubani huyo ambaye ana asili ya Uingereza alikasirishwa na kitendo cha watoto na raia wengine kuisogelea ndege aliyokua amepaki na huku askari huyo akiwa anashuhudia bila kuwatawanya watu hao ndipo rubani alikwenda kwa hasira na kumtolea maneno machafu na kudiriki hata kumsukuma huku watu wakiwa wanashuhuda tukio hilo. |
Asari huyo aliripoti polisi lakini hakuna hatua ambazo zilichukuliwa,wakenya wengi walisambaza video hiyo kwenye mitandao ya kijamii ndipo Kamanda wa polisi alipo muagiza rubani huyo kujisalimisha polisi kwa hiyari yake.Kwa mujibu wa sheria za kenya zinaeleza kuwa kosa kama hilo la kumdharilisha polisi adhabu yake ni kifungo kisichopungua miaka 10 au faini isiyopungua milion 1 ya kenya sawa na milion 20 za kitanzania.
USISAHAU KUACHA KOMENT YAKO THEN SHEA NA WANA