Wiki kadhaa zilizopita zilizagaa story kuhusu wema kuwa mjamzito lakini story hizo ziligeuka kuwa kweli mara baada ya wawili hao kuthibitisha kuwa wanasubiri kuitwa baba na mama na wakaelezea hadi ujauzito huo ulivyoingia,Lakini kuna baadhi ya mashabiki walibaki kuamini kuwa zilikua ni kick na sio ujauzito,Msanii ney wa mitego alienda mbali hadi kumuuliza swali wema kupitia wimbo wake mpya #SHIKA ADABU YAKO na kumuuliza je kweli ni mimba au anatafuta kiki za msimu?
Ni wiki sita tu tangu wema kutangaza mjamzito usiku wa kuamkia Leo 17 February story zilibadilika mara baada ya Idriss sultan kuandika shairi maarufu inaloitwa Latter to my unborn child,shairi hilo linazungumzia baba ambaye alikua anasubir watoto wazaliwe lakini haijawa hivo.Maneno hayo yalitafsiriwa kuwa huenda mimba ya wema imeharibika.
Lakini wakati bado watu wanajiuliza mchana wa leo Wema nae aliweka picha ya watoto mapacha na kuandika kuwa anashukuru kwa kila jambo linalotokea na hatochoka kujaribu.
Ney nae yamukuta makubwa kwa ilichoelezwa kuwa anamdomo mbaya kwa kile alichoimba kwenye wimbo wake ambao nimekuwekea hapo chini kipande kilicho muhusu wema.
TL inawapa pole Idrisa na mpenzi wake Wema kwa mtihani huo.
[soundcloud src="247516787"][/soundcloud]