Ni pale unapokuta na msichana usiyemjua lakini kwenye maongezi yenu anakuchangamkia kama mtu unaye fahamiana kabla,ofcoz utajisikia poa sana na kujikubali lakini ukweli ni hutokea baada ya manzi kukuelewa na hivi ndio vitu wanawake wanaviangalia kwa mara ya kwanza. |
1.UNANUKIA POA?
Hiki ni kitu cha kwanza kwa mwanamke kumkagua mwanaume anapomuona kwa mara ya kwanza,kuna wana wanajiita wasolid hivo wao kila kitu sio lazima tena hasa kwenye maswala ya kupendeza,sasa usijichanganye siku ya kwanza unakutana na msichana unatoa harufu ya ajabu nakuahidi hatokutafuta tena na atakuona bado hujielewi,acha usolid usio na maana pakupendeza pendeza kweli kuna mambo mengine sio ya usolid utakosa watoto wakali mwana.
2.UNAJALI MWILI WAKO?
Wanawake wanapenda mwanaume anayejali mwili wako vitu kama kucha na meno huwa vinawakosesha points vijana wengi sana,kwa kawaida hujui leo kwenye mizunguko unakutana na nani hivo ni jambo la msingi kuhakikisha muda wote unakua msafi sio tu kwa ajili ya washori ila kwa ajili ya afya yako pia.
3.UMEVAA NINI?
Najua utanijibu nguo,nguao kila mtu anavaa swali ni kwamba unapangilia vipi mavazi yako,haikuhitaji nguo za gharama sana ila zinaendana na ww?kuwa makini na rangi zako pia jitahidi kuwa na mavazi simple.
4.UNAJIAMINI KIASI GANI?
Naomba nikwambie kuwa kujiamini ni silaha tosha itakayoweza kukufanya ubebe mtoto mkali hata kama siyo level yako i mean kiumri au hata kipesa,kujiamini huanzia kwenye kutembea,unavyoongea na hata unavyosimama mbele yake,jifunze kujiamini na upunguze aibu,manzi akijua kama unajiuma uma hakika umemkosa.
5.JE MREFU KIASI GANI?
Haijalishi mrefu kiasi gani ila je unafurahia kimo chako,kwenye swala la urefu wanawake wengi hua wanatofautiana kuchagua na kama umetimiza hivyo vya juubasi ufupi au urefu sio tatizo ishu ni kwamba uwe wa kujiamini na sio kujistukia.
ENDELEA KUKAA KARIBU NA MWANAO WA DAMU KWA MADINI MENGINE USIACHE KUSHEA NA WANA.