Mahakama kuu Kanda ya Mtwara imeendelea kusikiliza pingamizi katika
Kesi ya uchaguzi inayomkabili Mbunge wa Jimbo la Ndanda Cecil Mwambe
iliyofunguliwa na aliyekuwa Mgombea wa Chama cha Mapinduzi CCM Mariam
Kasembe kwenye uchaguzi uliofanyika Oktoba mwaka jana.
Mariam Kasembe amemtuhumu Mbunge wa Jimbo la Ndanda kwa kuingilia
muda wake katika mikutano, kutoa lugha za kumdhalilisha pamoja na kuiba
Kura.
Katika Kesi hiyo ya Uchaguzi inayosikilizwa na jaji Dr Fauzi Twaibu
kwa Ombi la aliyekuwa Mgombea wa kupitia CCM mariam kasembe na kutuhumu
kuwa alidhalilishwa kwenye kampeni kwa kuambiwa kuwa yeye ni mchawi na
Alimuua mwanaye, ni mwizi na aliiba kura katika kipindi cha kura za
maoni ndani ya CCM na elimu YAKE NI ndogo ameishia darasa la Tatu.
Wakili anayemtetea Mbunge wa Ndanda Cecil Mwambe Tundi Lisu amesema
Tuhuma Hizo hazijaeleza Maeneo,Muda na siku gani Mtuhumiwa alitoa
maneno hayo ya kuudhi kinyume cha taratibu za sheria ya uchaguzi.
Hata hivyo Wakili wa kampuni ya Derost Elphance Rweshabula amesema
bila ya kujali muda kutokana na muda wa kampeni kujulikana Mtuhumiwa
alitoa Lugha ya Kuudhi kwa mteja wake hivyo mahakama inapaswa kutenda
haki.
Kwa mujibu wa Jaji wa mahakama kuu Kanda ya Mtwara
Dr. Fauzi Twaibu Pingamizi la kesi hiyo itatolewa Uamuzi wake tarehe 1
ya mwezi Tatu.
|
LISSU AMBANA MBUNGE WA CCM MAHAKAMANI HIKI NDICHO ALICHOAMUA HAKIMU
20:14
0
Tags