Ni muda mrefu sasa wanafunzi wa elimu ya juu wamekua wakilalamikia bodi ya mikopo hapa nchini,hatimaye kilio kimesikika na wamekuja na njia hii.
Bodi ya mikopo ya elimu ya juu nchini imesema kwasasa
imekwishaimarisha mifumo yake ya kupokea na kushuhulikia malalamiko ya
wanafunzi haswa kwa waliokosa mikopo kwenye bodi hiyo.
Hayo yamebainiswa na meneja wa habari, elimu na mawasiliano wa bodi
hiyo Bwana Omega Ngole huku akisema bodi hiyo kwasasa imejipanga vyema
katika kuhakikisha wanafunzi wanaomba mikopo wanapata mikopo kwa wakati.
Bwana Omega Ngole ametoa wito kwa mafisa mikopo wa vyuo hapa nchini
kuhakikisha wanabainisha matatizo ya wanavyuo na kuyashuhulikia kwa
wakati ili kupunguza migogoro ya wanavyuo hao katika upatikanaji wa
mikopo.
USIACHE KUCOMENT THEN LIKE ILI USHEE NA WANA