Baada ya kikao kilichofanyika hapo jana hii ndio kauli ya ACT WAZALENDO, |
Chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT - Wazalendo)
katika kikao chake cha Kamati Maalum ya Zanzibar cha tarehe 19 Februari,
2016 kimepokea taarifa rasmi kuwa aliyekuwa mgombea wa urais wa
zanzibar ndugu Khamis Idd Lila kwa kushirikiana na ndugu Ali makame Issa
huku wakitambua msimamo wa Chama kwa makusudi wameamua kupingana na
msimamo huo kwa maslahi yao binafsi na kukidhalilisha na kuingiza
mgogoro usiokuwa na sababu kwa kuandika barua ya kushiriki uchaguzi wa
marudio ambao Chama kilishapeleka barua rasmi tarehe 09 Februari,2016 ya
kutoshiriki uchaguzi hiuo.
Kwa kitendo chao hicho na kwa mujibu
wa Katiba, Kanuni na maadili ya chama Kamati maalum ya Zanzibar
imewasimamisha rasmi uanachama kwa mujibu wa katiba ya ACT Ibara ya 11
(2) kuanzia leo tarehe 19 Februri,2016 kwa ukiukwaji mkubwa wa katiba
Ibara ya 7(3)(5)(9),ibara ya 10 (2)(c)(d),Ibara ya 22(1)(2)(4).
Kwa mujibu wa Katiba ya ACT Wazalendo masuala yote ya kinadhamu kwa
viongozi na wanachama yanashughulikiwa na Kamati za uadilifu za ngazi
husika na kwa kuwa kwa sasa Kamati hizo hazijaundwa Kamati ya Uongozi ya
Taifa ndio inayoshughulikia na mambo yote ya kinidhamu.
Hivyo
jambo hili linawasilishwa mbele ya Kamati ya Uongozi ya Taifa kwa hatua
zaidi na kwa taarifa zaidi naambatanisha na tamko la Chama katika kikao
cha tarehe 13 Februari,2016 kilichofanyika Dar es Salaam.
Imetolewa leo tarehe 20 Februari, 2016
Juma Said Sanani
Naibu Katibu Mkuu
Zanzibar
Naibu Katibu Mkuu
Zanzibar
JE NINI MAONI YAKO? USIACHE KUCOMENT THEN SHEA NA WASHIKAJI