WANAWAKE:VITU VINNE USIVYOTAKIWA KUFANYA KWENYE NJIA YAKO YA UZAZI [UKENI] NI HATARI KWA MWANAMKE

Sungura17
0
 
Hivi karibuni kumekua na malalamiko mengi toka kwa wasichana kutopata ujauzito na wengine kutofurahia pale wanaposhiriki tendo la ndoa.Wanawake wengi hasa wenye umri kati ya miaka 18-45 wamekua wakikumbwa na matatizo mbalimbali ya uzazi bila kujua kwamba kwa namna moja ama nyingine wao wenyewe ndio chanzo cha matatizo hayo.
Leo tumekusogezea taarifa na tahadhari zilizotolewa na madaktari wakubwa nchini marekani ambao wameeleza mambo gani ya kuzingatia na kutothubutu hata kujaribu kwa kulinda afya ya uzazi na kutoharibu Uke wako.
1.VAGINAL DOUCHING
 Hii ile tabia ya kuosha sehemu za ndani ya uke kwa kutumia viosheo maalumu vinavyopatikana madukani au supermarket mbali mbali,Hapana hii ni tofauti na ule unawaji wa kawaida au uoshaji wa kawaida unapokwenda kuoga,haijakatazwa kuosha uke wako kwa maji ya uvuguvugu kwakua hiyo ni salama na haina matatizo kiafya.Vagina douching ni kule kutumia sabuni za maji au maji maalumu ambayo yanakua yamechanganywa na iodine,vinegar na magadi na kuyaingiza ndani ya uke,Hii ni hatari kwa afya ya uke wako.Njia bora ya kujisafisha ni kutumia maji ya uvuguvugu pale unapooga kwa kusafisha sehemu za nje na sio ndani ya uke kwakua inaelezwa kwamba uke hua unajisafisha wenyewe kwa na kutoa kitu kinachoitwa mucous ambayo ina control damu na uchafu mbali mbali ndani ya uke ameeleza Constance Young Daktari na profesa katika chuo cha Columbia University.
2. INSERTING UFOs
 Najua unafahamu kipi kinatakiwa kiingie na kipi kisiingie kwenye njia yako ya uzazi[ukeni],vidole,uume, na vifaa vya hedhi sio tatizo kiafya ila kumekua na tabia kwa baadhi ya wanawake kutumia ndizi,na vitu vinavyofanana na hivo katika kile kinacho aminika kujiridhisha pale anapokua mbali na mwenzi wake,Kama hujawahi kufanya tafadhari usijaribu na kama unafanya acha mara moja vitu hivi Husababisha vaginal irritation ni maumivu katika uke na michubuko ambayo itakufanya usifurahie tendo la ndoa.
3.SELF MEDICATING
DR.Dardik ameeleza kuwa tabia ya kujitibu bila kuwaona madaktar wa matatizo ya wanawake si jambo zuri kwakua imesababisha matatiz makubwa kwa wanawake wengi,ameeleza kuwa kuna wanawake wanatumia vitunguu swaumu,limao na wengine hata sabuni bila ya kufata utaratibu na ushauri wa daktari.Uke umejumuisha bakteria wabaya na wazuri wote hao wanakazi maalumu ya kufanya usawa wa homoni ukeni,matumizi ya madawa makali husababisha uwepo wa bakteria wabaya na hatimaye mwanamke anaweza kuona siku zake za hedhi haziendi sawa na wengine kutokwa damu nyingi na maumivu makali wanapokua katika mzunguko,Alisema.
4.VAGINAL STEAMING

 Hiki ni kitendo cha kujifukiza kwa marashi,kumekua kiaminika na baadhi ya matabibu wa asili kutokea nchi za uchina,korea na japani ambao wameambukiza hadi mataifa kama marekani na uingereza tendo hili huitwa vaginal steaming huchukuliwa marashi yanaitwa VAGI-STEAM na mwanamke hukaa juu ya kiti ambacho chini yake kuna bakuri yenye maji yamoto na mvuke huo huenda moja kwa moja kwenye sehemu za uke,Jambo hili hufanywa kwa nia ya kusafisha uke lakini  imepigwa vita na madaktari wakieleza kwamba si sahihi kwani huwaondoa baadhi ya bakteria wanaotakiwa katika kurekebisha mfumo wa homoni na kusababisha madhara katika afya ya uzazi.

Share na jamaa zako ili na wo wapate kujua na kubaki salama na afya zao.
Endelea kukaa karibu na Website na Tanzaline.blogspot.com
Tags

Post a Comment

0Comments

Post a Comment (0)

#buttons=(Ok, Go it!) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Ok, Go it!