Siku chache baada ya kuripotiwa tukio la utunguaji ndege lililofanyika katika pori la tengefu la maswa wilayani meatu mkoani simiyu na
kusababisha kifo cha rubani wa chopa hiyo huku rubani mwenzie
akijeruhiwa vibaya mguuni hatimaye Hakimu mfawidhi wa Mahakamaya wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu Mary Mrio ametoa hukumu kwa kesi ya tatu inayowakabili watuhumiwa saba ambayo ni kukutwa na silaha kinyume cha sheria,Hata hivo mara baada ya maelezo ya wakili mahakamani hapo, watuhumiwa wote wanne kati ya saba walikiri kutenda makosa hayo, ambapo wote waliiomba mahakama kuwapunguzia adhabu kwa kile walichoeleza kuwa ni mara yao ya kwanza kutenda makosa kama hayo.
Lakini wakili Mlekano aliitaka mahakama kutoa adhabu kali kwa watuhumiwa wote ili kuwa fundisho kwa watu wengine wenye nia ya kutenda makosa kama hayo.Na ndipo hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo ya wilaya alisoma hukumu ya kwenda jela miaka 60 kwa watuhumiwa hao.