Jacqueline Ntuyabaliwe ndilo jina la kwenye passport ya Mrenbo huyo aliyewahi kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss world miaka ya mwanzoni mwa 2000.Kylnn ambaye kwa muda Mrefu hakuwa kusikika na akiwa sio mtu mwenye kupenda kuzungumzia mambo yake ya kifamilia wakati ambao watu wanamzungumza vibaya juu yake Na amekua akijulikana kwa jina la Bossylady asiyependa makuu,Leo hii aliandika ujumbe mzito kupitia ukurasa wake wa Instagram
ambao unatafsiriwa kwamba ni ujumbe kwa wale ambao wanamzungumzia kuhusu ndoa yake na mfanya biashara mkubwa hapa nchini DR.REGINALD MENGI,kwa marfu kabisa Kylnn ambaye ni mama wa watoto wawili aliandika haya,
Kama ambavyo binaadamu hatuwezi kuona ndani ya moyo wa mtu na tunakubali na kuheshimu hilo vilevile tujifunze kukubali na kuheshimu na kukubali yale tunayoyaona nje ambayo ni matokeo ya hisia za moyo.Kwa mfano,usimshangae wala kumdhihaki au hata kujaribu kumtafutia sababu au maelezo ya kwanini aliyeoa/kuolewa na mtu mwenye aidha ulemavu wa aina yoyote,kabila/taifa ambalo kwako unaliona ni tofauti.Upendo ni chaguo binafsi na kama ambavyo ungependa chaguo lako lisiingiliwe ndivyo ilivyo kwa kila binadamu wenzako.Tukielekea katika kusherekea siku ya wapendanao (Valentines Day) naomba tufahamu kwamba kila binadamu anastahili upendo bila kujali kabila,umri,hali ya ulemavu na hata uzuri au ubaya wa sura au maumbile na tufahamu kuwa hata huo uzuri au ubaya unatofautiana kutokana na mtu aonavyo.Uhuru wa Upendo utawale siku ya Valentines na siku zote za maisha yetu.
Licha ya kwamba Mwana mama huyo si mtu wa kusikika katika medias ila amekua anatumia sana mtandao wake wa instagram kueleza yale yanayo mgusa na hata mambo anayofanya kama vile familia,kazi na mengineyo.
[gallery] [img src="https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgv8YAybfPHyX3D-29ckLJF8MjvxJT_qSDZQTcpl8cnhwIvtS_lBIspZzGHdpT9MZGY-vb4rVmAqjBhbe4nZPeAzIhQdcwT-jopqFv7PnPQGV2k3slt_vFz0ehjHgVq8mSrjpvmIm2CrGY/s1600/kylnn+swim+tanzaline.jpg"][/img] [img src="https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi3dmDoIAx-bCgrAHO1CgoVR07I76oj8AM17epGYsWxGsl85oVZyRsUySKGi3M9LuHweEa6tf7FM_ltCtk14jtrha6EgcbTsovEm0KHaLo_5J_R5kZE7a-B9hqHuh_gBszAN8M1HGlNfBw/s1600/kylnn+tanzaline.jpg"][/img] [img src="https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgh0JbPIYlQrkZgmGhRZwRwBFmEcQGpR17tM-iBwjQ-9nNHowHOfnwqzgFz1n81q_5hz3yjjXH3DO_xAfuRSn6dsP5VGcpVAfO8nAfaNjxo_geC-Zl1g2qvJiJingiFAI7GRJvIDaR6gCY/s1600/mengi%252Ckylnn%252Cwatoto+tanzaline.jpg"][/img] [/gallery]