BREAKING NEWS:WAZIRI MKUU AWASIMAMISHA KAZI WATENDAJI WAKALA WA VIPIMO TANZANIA

Sungura17
0
Hapo jana 12 february mheshimiwa waziri mkuu alipofanya ziara ya kushtukiza bandarini


 Ikiwa bado Mzimu fukuza fukuza unaendelea kuikumnba mamlaka ya bandari hapa nchini hapo jana alhamisi 11/2 mheshimiwa waziri mkuu alifanya ziara ya ghafla bandarini hapo na kukuta makosa mengi ya kiutendaji yakiwa bado yanaendelea kufanyika licha ya kwamba mamlaka hiyo imekua ikipata ziara hizo mara kwa mara tangu kuapishwa kwa raisi JOHN POMBE MAGUFULI.
Katika ziara hiyo mheshimiwa kassim majaliwa  alimpa saa nne tu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo nchini (WMA), Bi. Magdalena Chuwa aandike barua ya kujieleza ni kwa nini aliamua kufunga mita hizo zisitumike kwa zaidi ya miaka mitano iliyopita na aipeleke barua hiyo ofisini kwake ifikapo saa 11 jioni jana.
Leo taarifa kutoka Ofisi ya waziri mkuu zenye makao makuu mtaa wa magogoni Dar es salaam zinaeleza kama ifuatavyo
SERIKALI imeamua kuwasimamisha kazi watendaji wawili kutoka Wakala wa Vipimo nchini (WMA) kuanzia leo ili kupisha uchunguzi wa upotevu wa mafuta bandarini kutokana na zuio la kufunga kwa mita kwa zaidi ya miaka mitano.
Waliosimamishwa kazi ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo nchini (WMA), Bi. Magdalena Chuwa na Meneja Vipimo Kitengo cha Bandari, Bi. Bernadina Mwijarubi. Bi. Mwijarubi ndiye anashughulikia kitengo cha mafuta bandarini.
Akitangaza uamuzi huo kwenye kikao cha Makatibu Wakuu kilichofanyika leo (Ijumaa, Februari 12, 2016) ofisini kwake Magogoni jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemwagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dk. Adelhelm Meru awaandikie barua za kuwasimamisha kazi ili kupisha uchunguzi huo.
“Katibu Mkuu Viwanda, waandikie barua za kuwasimamisha kazi ili kupisha uchunguzi. Katika kipindi hiki hawatatakiwa kusafiri kwenda popote hadi uchunguzi utakapokamilika. Pia utafute mtu wa kukaimu nafasi hiyo ili kazi ziendelee,” alisema.
Waziri Mkuu pia amesema ofisi yake itawaandikia barua ofisi ya TAKUKURU na polisi ili wafuatilie suala hilo mara moja na ikithibitika kuwa walihusika hatua rasmi zitachukuliwa na itathibitika hawakuhusika basi watarudishwa.
Waziri Mkuu pia aliagiza mfumo wa upimaji mafuta kwa kutumia flow meters uendelee kutumika na ule upimaji wa kukadiria uache kutumiwa mara moja.

MHESHIMIWA WAZIRI MKUU AKIKAGUA MITAMBO YA UPIMAJI MAFUTA HAPO JANA TAR.11/2

Tags

Post a Comment

0Comments

Post a Comment (0)

#buttons=(Ok, Go it!) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Ok, Go it!