Hali ya sintofahamu ilitanda mkoani Iringa mara baada ya watu zaidi ya 3000 tarafa ya pawaga wilaya ya iringa vijijini kuzungukwa na maji ya mafuriko ambayo yanaelezwa kuwa na vimelea vya kipindupindu ambacho bado kinaendelea kuutesa mkoa,Maji hayo yalizingira vibanda zaidi ya 50 ambavyo vilikua vikitumika na wakulima katika vitongoji vya mboliboli na kimande na yakapelekea watu hao kukosa msaada wa chakula kwa siku mbili.
Leo mchana bi amina masenza alieleza kuwa muda si mwingi helikopta kutoka Dar es salaam kuwa ingewasili mkoani hapo kwa ajili ya msaada wa chakula lakini pamoja na kufanya uokoaji wa wakulima hao ambao inasemekana wengi wao ni wakazi wa Morogoro na Mbeya.
Hatimaye ufumbuzi umepatikana mara baada ripota wetu kushuhudia helikopta hiyo ya polisi yenye bamba 5H-PAW ikiwasili mkoani hapo Jioni tayari kwa kuanza uokoaji.
[gallery] [img src="https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjYtTlijlKgp_SRWFLoGYqqUmjMNfhcveq_GKjGB_bYWACFQoItdKZiA8fQbAiDq1K2ODg65xRYSJr3Lt-4xtlR-DDKL68tPi-gprd2D36lO2YqGYzdbBNgEFfvuTMBihhyphenhyphenp6YVV5DeP0Q/s1600/HLKPT2.jpg"][/img] [img src="https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgDRHKtTbBvL5B67ize43zhUjO_ZRi645H-RfB63epF6KluxHGpNvFN_6Fl9jRwrkS9RE5jSZ-SapGgzsDLvKfz8ky9MywLRAdQX9vaykCi-6vaWGvz5GbKkpqdScwBTvHUZFjtfvjp5pc/s320/HLKPTAA.jpg"][/img] [img src="https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEikLz9HqYlrn7GwKv9-clTFtJeTXxH9XL3mQpiWBLReX7FtzIwlO1Mn4cOfkOQ3_R_xlSqKCNIs0Q87bFXMYGCC9xiF3JiZ6fTz9rMhGv9_-q4ic3372oy7tXdTeDExdhlM1rVAsIo98nA/s320/PLS.jpg"][/img] [/gallery]