Huenda ukawa unafahamu kuwa Ndugu wawili wanaounda kundi la P'square yani peter okoye na paul ni mashabiki wakubwa wa mpira wa miguu,Mara nyingi Peter amekua akiweka picha akiwa amevalia jezi za chelsea na huenda ukawa unafikiria ni shabiki tu wa kawaida lakini leo acha nikujuze kitu ambacho huenda ukawa hukifahamu,
Peter okoye Hivi karibuni alikua london ambako alienda kucheki mechi kati ya CHELSEA VS MAN U baada ya mechi alikutana na baadhi ya wachezazaji wa timu hiyo akiwepo Oscar,Hazard,willian, Nemanja Matic na Mnigeria mwenzie Mikel obi.Usichokifahamu ni kua si tu kwasababu anaipenda chelsea lakini pia furaha yake kubwa ilikua kukutana na Jamaa ya ambaye kama sio mziki basi wangekua wote katika soka la ulaya kwakua ,
ndoto ya Nyota huyo ilikuwa ni kucheza soka na kabla hajaanza harakati za mziki alikua anakipiga katika Academy moja na Nyota wa chelsea mikel obi miaka 20 iliyopita,anasema anafurahi kumuona mshikaji wake akiwa anacheza soka la kimataifa na kusema hata yeye alikua anatamani kufika huko ila mziki ndio kazi aliyopangiwa na mwenyez mungu.Haya bwana peter kweli mziki ni kazi uliyopangiwa na mungu huenda ungepiga soka tusingekujua au usingetupa utamu tunaopata kwenye mziki wako,Tazama baadhi ya picha alizopiga na wachezajia wa chelsea alipokua uwanjani hapo.