Wenye umri wa miaka 65 kwa hapa kwetu asilimia kubwa ni baba na mama zetu na wengine huenda ukawa umri wa babu au wa bibi yake.Hivo basi ndege huyu anayeitwa Laysan Albatross wisdom
,Huenda akawa na umri sawa na Mama,baba,bibi au babu hivo anastahiki Kupewa shikamoo kwa umri alionao.Imethibitika kuwa ndege huyu ndiye mwenye umri mkubwa zaidi duniani umri wake ni miaka 65 .Hii ni wiki ya Furaha kwa ndege huyu kwani ameanza maisha mapya ya kuitwa Mama kwa kujipatia kifaranga hapo Jana.
Kama bado hujui ndege huyu ameruka umbali wa takribani maili Milion 3 tangu aanze kufatiliwa mwaka 1956.