Katika hali isiyo ya kawaida mfanyakazi wa shirika la umeme hapa nchini Tanesco,Amejikuta akiingia katika Matatizo pale ambapo wananchi wa Lumuma wilayani kilosa Mkoani mororogoro walipofunga barabara kuzuia gari lililokua likielekea kijiji jirani kusambaza umeme.
Shuhuda mmoja alieleza haya"Kwa muda mrefu hatuna umeme katika eneo hili lakini cha kushangaza Tanesco wanapitisha nguzo zao katika mashamba yetu kupeleka umeme vijiji vingine na hapa kwetu hatuna umeme au sisi sio watanzania? alihoji Mkazi wa kijiji hicho.