Unaweza sema Korea kaskazini moja ya mpango wao mwaka huu ni kujitoa umoja wa mataifa,kwakua tangu mwaka uanze kumekua na hali ya sinto fahamu hasa mahusiano kati ya umoja huo na jamhuri ya watu wa korea kaskazini.Sinto fahamu hiyo inakuja mara baada ya urushwaji wa makombora ambao umezua mgogoro bainaya pande hizi mbili hapo nyuma Tarehe 8 February umoja wa mataifa kupitia Barza la usalama lililazimika kuweka kikao cha dharura kuijadili korea kaskazini kwa kile kilichoitwa kukiuka makubaliano ya amani kwa kurusha kombora lililodaiwa kuwa ni jaribio la nyuklia hapo tarehe 7 February.
Lakini licha ya vitisho vya baraza la usalama la umoja wa mataifa kueleza kuwa watachukua hatua kali dhidi ya korea kaskazini.Leo Raisi wa korea kaskazini akiongea kupitia televisheni ya Taifa kwa ubabe ameagiza na kusisitiza kuwa wanasayansi nchini humo waendelee na kazi yao kama kawaida huku akieleza kuwa wanaotaka nchi yake ikwame hakika hawatoweza matarajio yake ni kuiona nchi yake inasonga mbele.Swali ni kwamba ni uamuzi gani umoja wa mataifa utachukua dhidi ya Korea kaskazini?