Msanii wa bongo movie Vicent kigosi(RAY) mara baada ya kuzingirwa na kila aina ya kijembe kwenye mitandao ya kijamii,Leo kupitia kipindi cha Leo tena cha Clouds FM ray alieleza kinaga ubaga kuhusiana na kuishi kwao na kujichubua Ray alisema haya.
‘’Mimi sijichubui
nakunywa sana maji na kufanya mazoezi namshangaa sana Nay kuniambia
natumia pesa zangu za mauzo ya filamu kununua mkorogo sio kweli ni
maisha tu ndio yamenibadilisha namshukuru Mungu sipingwi na jua ndani ya
gari kuna AC,nyumbani AC na ofisini AC lazima uwe mweupe,’’RAY liendelea na kusema
‘’Maisha ya
zamani ya wasanii ni tofauti na sasa zamani msanii alikutembea juani kwa
muda mrefu ndio maana tulikuwa tunaonekana weusi,Halafu sisi kwetu
hatuna asili ya weusi ni maji ya kunde ,
‘’Ni kweli naishi
nyumbani na kuishi kwetu sio kama sina nyumba na kuishi nyumbani sio
dhambi ,kujitegemea ni maamuzi yako binafsi,mimi naishi nyumbani na mama
yangu ni mtoto wa mwisho lakini huwa sipendi kujionyesha nina utajiri
gani sipendi kupost mali zangu,sijui nina nyumba ,magari ni ishu zangu
binafsi,kila msanii ana stlye yake ya maisha mwingine anapenda
kujionyesha kwenye mitandao na mali gani,’’
JE,UNASEMAJE KUHUSU RAY?NI SAHIHI KUISHI NA MAMA KWA UMRI WAKE NA VIPI KUHUSU KUJICHUBUA MAJIBU YAKE UMERIDHIKA NAYO?USISAHAU KUACHA COMMENT HAPO CHINI SHEA NA WASHIKAJI...