Mshambuliaji
hodari wa Real Madrid Cristiano Ronaldo amezua mjadala mkali baada ya
kutoa matamshi yaliyoonekana kulaumu wachezaji wenzake baada ya
kushindwa nyumbani 1-0 na Atletico Madrid hapo jana (Jumamosi).
"Tungekuwa wa kwanza iwapo wachezaji wote wangeweza kucheza kama mimi,"
Ronaldo aliambia waandishi wa habari. "Sitaki kukosea mtu heshima,
lakini ni vigumu kushinda wakati wachezaji bora hawako
uwanjani," alisema akionekana kufedheheshwa. "Ningependa kucheza na
Pepe, Karim, Gareth Bale...Marcelo... Sijasema kuwa Jese, Lucas na
(Mateo) Kovacic ni wachezaji duni." alisema Cristiano.
Matamshi ya Ronaldo yamezua hisia mbali mbali kwenye mitandao ya jamii na kugonga vichwa vya habari za spoti duniani.