Baraza la usalama la umoja wa mataifa limelaani vikali urushwaji wa kombora uliofanywa na jamuhuri ya watu wa korea kaskazini hapo jana 7th February kwa kuuita ni ukiukwaji wa makubaliano ya kimataifa na mkataba wa amani na usalama.
Leo hii 8th Feb limelazimika kukaa kikao cha dharura katika kulijadili swala hilo ambalo linalotia wasi wasi kiusalama Kwakua kitendo hicho kinaripotiwa kuwa ni nuclear test na sio satelite kama N.KOREA wanavyodai.
Mara baada ya kikao hicho mwakilishi wa kudumu wa umoja wa mataifa ambaye pia ni raisi wa baraza hilo la usalama la umoja wa mataifa ameongea na waandishi wa habari na haya ndiyo aliyozungumza,
Wanachama wote wamesisitiza kuwa kitendo kilichofanywa na N.KOREA ni ukiukwaji wa mkataba wa amani na pia ni uvunjwaji wa makubaliano ya kimataifa dhidi ya nuclear,wanachama wameeleza kuwa hata kama urushwaji wa kombora hilo unalinganishwa na urushwaji wa satelite na vyombo vya angani Wao bado wanaona si sahihi kwani imekua ni tabia ya kujirudia kwa Taifa hilo lakinipia matumizi ya teknolojia ya Balistiska sio sahihi kulingana na makubaliano ya kimataifa yaliyowekwa nchi wanachama. Alisema kiongozi huyo RAFAEL DARIO RAMIREZ CARRENO.
Lakini pia baraza hilo limeapa na kuahidi kuunda na kusimamia kikamilifu Azimio jipya katika kukabiliana na makosa kama hayo yanayofanywa kimakusudi ikiwa ni hatari kwa dunia.
Swali linabaki kuwa hatua gani itachukuliwa na U.N lakini upo uwezekano mkubwa Nchi hiyo kuwekewa vikwazo vya kiuchumi japo kua Taarifa hiyo ya Mh.Ramirez haijaeleza moja kwa moja,kitendo hicho kimekua ni tabia ya kujirudia inayofanywa na taifa hilo ikumbukwe urushwaji wa aina hiyo ulifanywa mapema mwaka huu Tarehe 6 January.
JE,kipi N.KOREA watakacho amua na wao kulingana na hatua ambazo zinatajwa kuchukuliwa dhidi yao,ikiwa wao wamekanusha kua sio majaribio ya Nuclear ni Satelite.