Kuelekea mchezo wa jadi jumamosi hii,Shilikisho la mpira hapa nchini limetoa viingilio vya mchezo huo ambao utapigwa majira ja saa 10 jionii kwa saa za hapa kwetu,TL imekusogezea taarifa hiyo kama ifuatavyo
Kiingilio cha chini kitakua shilingi elfu 7 tu na kiingilio cha juu kitakua shilingi Elfu Thelathini
(30,000) kwa VIP A, Elfu Ishirini (20,000) VIP B & C, Elfu Kumi
(10,000) kwa viti vya rangi ya machungwa (Orange), na Elfu Saba (7,000)
kwa viti vya rangi ya bluu na kijani.
Tiketi za mchezo huo zitaanza kuuzwa siku ya Ijumaa saa 2 kamili
asubuhi katika vituo vya TFF (Karume), Buguruni Olicom, Ubungo Oilcom,
Kidongo Chekundu (Mnazi Mmoja), Posta (Agip), Dar Live (Mbagala), Uwanja
wa Taifa, Makumbusho Stand, Kivukoni Ferry.
Mchezo huo utachezeshwa na waamuzi wote wenye beji za FIFA, mwamuzi
wa katikati Jonesia Rukyaa (Kagera), akisaidiwa na Josephat Bulali
(Tanga), Samwel Mpenzu (Arusha), mwamuzi wa akiba Elly Sasii (Dar) huku
Kamisaa wa mchezo huo akiwa Khalid Bitebo (Mwanza).