Freedom 251 huenda ikawa ndiyo smartphone itayouzwa kwa wingi kuliko smartphone zote duniani kwa mwaka 2016 kutokana na kweli kwamba idadi kubwa ya watu duniani ni wale wenye kipato cha chini,Hapo jumatano kampuni ya RINGING BELLS ambayo ni kampuni changa kwenye soko la smartphone walizindua simu hiyo na kutangaza itauzwa kwa dollar 4 za kimarekani sawa na shiling 8700 za kitanzania,Watu hawakushangazwa sana na bei ila uwezo wake ndiyo uliowashangaza zaidi watu waliohudhuria tukio hilo,Freedom 251 ni simu ya line mbili,processor speed ni 1.3ghz,memory ya ndani ni GB 8,RAM GB 1,camera ni 3.2 megapixels,Front camera 0.3 megapixels.
Kampuni hiyo baada ya kutangaza kuwa wameanza kupokea oda za wateja ambao watapatiwa simu zao mwezi wa sita waka huu haikuchukua muda mrefu mtandao wao ulipata wateja zaidi ya laki 6 kwa sekunde kitu ambacho kiliwafanya wabadilishe mtandao wa manunuzi,Serikali imepokea tofauti swala hilo na kusema kuwa hawataruhusu simu hiyo iuzwe kwa bei hiyo na wamesema kuwa bei ya chini ya smartphone ni dollar 29 za kimarekani ambazo sawa na shilingi 63000 za kitanzania.Lakini bado tamko rasmi la serikali ya india haijawa wazi na kampuni ya Ringing bells inaendelea kupokea oda za simu hiyo ambayo inatoka rasmi mwezi wa sita mwaka huu.
SWALI NI JE SERIKALI YA INDIA IPO SAHIHI KUZUIA WASIUZE KWA BEI HIYO?USISAHAU KUCOMENT HAPO CHINI THEN SHEA NA WASHIKAJI.